DAWA YA BAWASIRI
Kifupi kuhusu bawasiri. Bawasiri katika mzunguko wa tundu la njia ya haja kubwa Ugonjwa huu wa bawasiri ni ugonjwa unaotokana na kuvimba kwa mishipa ya damu katika mfereji wa njia ya haja kubwa. Ugonjwa huu katika jamii hufahamika kwa majina tofauti tofauti hutegemea kabila na mahali. Ugonjwa huu umekua ni ugonjwa hatari kutokana na tabia za wagonjwa kuficha kutokana na aibu ya tatizo lenyewe lilipo au kuhofia jamii kumtazama tofauti kwa sababu jamii nyingi hasa za afrika mashariki zinaamini kuwa ugonjwa huu ni mkosi mkubwa. Kuna aina kuu mbili za bawasiri . 1.Bawasiri ya nje 2.Bawasiri ya ndani Bawasiri hii ya ndani ndio bawasiri mbaya kabisa kwa sababu ni vigumu mgonjwa kujitambua kua anatatizo na hii inatokana na tabia ya bawasiri ya ndani kutokua na maumivu wakati inaanza. SABABU ZINAZOPELEKEA MTU KUPATA BAWASIRI. Ugonjwa huu wa bawasiri husababishwa na mambo yafuatayo; 1.Tabia ya kuketi sehemu moja kwa muda mrefu mfano;madereva. 2.Tatizo sugu la kuharisha. 3.Ujauzito....