MALIZA KABISA TATIZO LAKO KWA MIMEA ASILIA
Fahamu Jinsi Ya Kutibu Magonjwa 21 Kwa Kutumia Tiba Asili.
1. Tiba ya miguu kuwaka moto.
Chukua majani ya mti wa Mvumbasi unguza pamoja na majani ya mti wa mnungunungu, halafu changanya na mafuta ya taa lita moja.
Matumizi:
Utakuwa unatumia kujichua kwenye miguu kutwa mara tatu kwa muda wa siku 15
2. Tiba ya kikohozi.
Tafuna majani ya mti wa mbaazi.
Mbali na kutibu kikohozi,mti wa mbaazi,unatibu magonjwa mengine mengi Mfano,mizizi ya mti wa mbaazi husaidia kutibu chango la kiume na kusafisha kibofu cha mkojo.
3. Kuvimba kwa tezi ya shingo.
Kama una sumbuliwa na tatizo la tezi
kuvimba, chukua unga wa Kamun Nyeusi kisha changanya na sega la nyuki, halafu tumia kukanda kwenye tezi kila siku kwa muda wa wiki 2.
4. Tiba ya maumivu ya mgongo, miguu, nyonga, na kifua kupasua.
Kama una sumbuliwa na maumivu ya mgongo, miguu, nyonga na kifua kupasuka
Fuata maelekezo yafuatayo:
Chukua mafuta ya nyonyo robo lita, mafuta ya Kamun Nyeusi kiasi cha robo lita pamoja na mafuta ya karafuu robo lita, changanya pamoja halafu uwe unatumia kujichua sehemu yenye maumivu, kutwa mara tatu kwa siku 15.
5. Tiba ya kwikwi.
Kama unasumbuliwa na kwikwi, fuata maelekezo yafuatayo.
Chukua majani ya mwembe mkavu, pekecha kisha mpe mgonjwa atumie kuvuta kama sigara halafu awe anameza moshi
6. Tatizo La Kukojoa Kitandani.
Kama una tatizo la kukojoa kitandani tumia mizizi ya mbaazi kwa kuchemsha na kunywa maji yake kutwa mara mbili kwa siku, kwa muda wa siku kumi na nne.
7. Tatizo la uvimbe kwenye kizazi.
Kama una tatizo la uvimbe kwenye kizazi chukua mizizi ya mtopetope tumia kwa kuchemsha na kisha kunywa maji yake, mara tatu kwa siku kwa siku 15
8. Vidonda vya koo.
Kama una tatizo la vidonda vya koo, chukua maji ya uvuguvugu kiasi cha nusu lita, kisha kamulia ndimu tatu fresh halafu tumia kusukutulia Utafanya hivyo mpaka utakapo pata nafuu.
9. Malaria sugu.
Kama una malaria sugu chukua maji ya dafu moja weka kwenye chombo kisafi kisha kamulia ndimu saba halafu tumia kunywa.
Fanya hivyo mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni kwa siku tatu hadi saba.
10. Tiba ya tatizo la kutoa harufu mbaya kinywani, sehemu za siri, kikwapa na jasho lenye harufu mbaya.
Chukua maji yaliyo lowekewa mchele kiasi cha lita moja, kisha tumia kunawia sehemu husika na kusukutulia mdomo, Utafanya hivyo mara tatu kwa siku hadi utakapo ridhika na matokeo unayo yahitaji.
11. Kwa wakina mama Jinsi ya kuzuia uchungu wa mimba, maumivu ya kiuno, maumivu wakati wa hedhi, na damu itokayo bila mpangilio wasiku maalumu,
Chukua majani ya mbigili yatwange halafu changanya na vijiko vitatu vikubwa vya unga wa mti unaoitwa msonobali kisha tumia kunywa glasi 1 yenye ujazo wa milimita 250 kutwa mara tatu hadi hali yako itakapokua nzuri.
12. Tiba Ya Vidonda Vya Tumbo, Kisukari pamoja na Typhoid.
Chukua mizizi ya mti wa msongati pamoja na majani ya mkalatusi vitwange kwa pamoja kisha chemsha kwenye maji lita moja,
halafu tumia kunywa glasi moja ya robo lita, mara tatu kwa siku kwa siku 15
13. Tiba Ya Tatizo La Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa Kwa Wanawake.
Kama wewe ni mwanamke unaye sumbuliwa na tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa,unaweza kutibu tatizo lako kwa kutumia vyakula mbalimbali kama ifuatavyo
i. Juice ya miwa.
Tumia kunywa nusu lita ya juisi ya miwa,mara tatu kwa siku asubuhi,mchana na jioni kwa siku kwa siku 16
Mbali na kuwasaidia akina mama wenye tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa, juisi ya miwa ina faida nyingine nyingi kitabibu.
Moja kati ya faida kubwa za juisi ya miwa,ni uwezo wake mkubwa wa kusafisha figo.Hivyo hata wanaume wanashauriwa kutumia juisi ya miwa au miwa kwa wingi kwa sababu inasaidia kusafisha figo,na figo ni moja kati ya ogani muhimu sana katika mfumo wa nguvu za kiume.
ii. Mbegu za fenesi.
Chukua mbegu za fenesi kiasi cha robo kilo kisha chemsha na maji lita mbili halafu tumia kula pamoja na supu yake, Utafanya hivyo mara tatu kwa siku kwa muda wa siku 16, Unaweza pia kuzisaga na kutumia unga wake kwa kuchemsha na kunywa kwa kufuata utaratibu huo hapo juu.
iii. Korosho.
Tumia kula korosho pakti moja yenye ujazo wa robo kilo mara tatu kwa siku, asubuhi, mchana na jioni kwa siku 16. Yaani asubuhi tumia robo kilo mchana robo kilo na jioni robo kilo kwa siku 16
iv. Mihogo mibichi.
Tumia kutafuna walau vipande vitatu vya mihogo mibichi kwa siku kwa muda wa siku 16 Yaani asubuhi utumie kipande kimoja kikubwa, mchana kipande kimoja kikubwa na usiku,utumie kipande kimoja kikubwa.
14. Tiba asili ya tatizo la kifua kubana kwa watoto waliokunywa uchafu wakati wa kuzaliwa,
๐pumu,
๐kifua kisichopona kwa watu wazima
๐Kichomi
๐kuwashwa mwili.
๐Na kupaliwa wakati umealala usingizi.
Tiba Yake.
Chukua majani ya mpera kiasi cha kama viganja vinne yaponde pamoja na magome ya muembe kiasi cha viganja vinne na tunda la komamanga twanga vyote kwa pamoja (Yani majani ya
mpera, magome ya muembe na tunda moja la komamanga) Ukisha maliza kutwanga changanya na maji lita mbili halafu chemsha pamoja na lita moja ya asali mbichi ya nyuki wadogo.
Chemsha hadi itokote, halafu ipua dawa yako.
Matumizi.
Kwa mtoto mdogo mwenye umri wa kati ya mwaka mmoja na miaka mitano, tumia kumpa kijiko kimoja kikubwa mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni kwa siku saba.
Na kwa mtu mzima tumia kunywa vijiko vikubwa viwili mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, kwa siku 10
15. Tiba ya tatizo la mtoto wa Jicho.
Kujitibu mtoto wa jicho tumia kunyunyizia jichoni matone mawili ya utomvu wa toto la ndizi. Fanya hivyo mara tatu kwa siku, asubuhi, mchana na jioni kwa siku 20.
16. Tiba ya kupunguza gasi tumboni, Tiba ya kiharusi na kifafa.
Chukua mizizi mitatu ya mti wa ukwaju mizizi mitatu ya mti wa mkungu, mizizi mitatu ya mpapai, pamoja na mizizi mitatu ya mti wa ufwambo.
Iponde ponde yote kisha chemsha kwa pamoja kwenye maji ya lita tatu hadi yachemke.
Tumia kumpa mgonjwa glasi moja, kutwa mara tatu kwa siku 19.
Chukua juisi ya kitunguu maji kiasi cha glasi moja yenye ujazo wa milimita 250, kisha changanya na asali mbichi kijiko kimoja koroga halafu tumia kunywa Utafanya hivyo mara tatu kwa siku kwa muda wa siku 14.
AU chukua kipande kimoja cha tangawizi kiponde ponde kisha chemsha kwenye nusu lita ya maji pamoja na kijiko kimoja kikubwa cha asali mbichi ya nyuki wadogo,
halafu tumia kunywa kutwa mara mbili kwa siku 21
Au Chukua asali mbichi ya nyuki wadogo kiasi cha robo lita, changanya na vijiko vitatu vikubwa vya unga wa Kamun nyeusi, kisha chemsha pamoja kwenye maji lita moja, Halafu tumia kula vijiko vikubwa vitatu kutwa mara tatu kwa siku ishirini na moja.
17. Tiba ya pumu.
Chukua magadi vijiko vikubwa vitatu, saga upate unga wake, kisha changanya na samli ya n’gombe vijiko 21 vikubwa na asali vijiko 30
vikubwa.
Matumizi.
Tumia kula vijiko vikubwa vitatu asubuhi, vitatu jioni na vitatu usiku kwa muda wa siku 20.
18. Tiba ya kiharusi na kifafa.
Chukua mizizi mitatu ya mti wa ukwaju, mizizi mitatu ya mti wa mkungu, mizizi mitatu ya mpapai, pamoja na mizizi mitatu ya mti wa ufwambo.
Iponde ponde yote kisha chemsha kwa pamoja kwenye maji ya lita tatu hadi yachemke.
Tumia kumpa mgonjwa glasi moja kutwa mara tatu kwa siku 21.
19. Tiba ya fangasi kwenye damu.
๐Ukurutu.
๐Upele.
๐Mchafuko wa damu Pamoja na kuwashwa mwilini.
Chemsha robo kilo ya majani ya mti wa mdimu kwenye maji kiasi cha lita mbili, Maji yakisha tokota,
ipua chuja halafu tumia kunywa glasi mbili asubuhi, mbili mchana, mbili jioni, Utafanya hivyo kwa muda wa siku 20.
20. Tiba ya fangasi za miguu na kunuka miguu.
Twanga majani ya mwarobaini robo kilo,chemsha na maji lita tano kisha weka kwenye beseni halafu loweka miguu yako ndani ya beseni kwa muda wa lisaa limoja.
Utafanya hivyo kutwa mara mbili kwa muda siku 10
AU chukua majivu kiasi cha robo kilo,changanya na robo lita ya juisi ya ndimu kisha nyunyizia kwenye miguu na ukae kwa lisaa limoja.
Utafanya hivyo mara mbili kwa siku kwa siku 10 Japo inauma lakini ni tiba nzuri sana.
21. Kuongeza maziwa kwa mama anaenyonyesha.
Chukua majani ya mti wa ukwaju, kiasi cha nusu kilo kisha chemsha na maji lita tano.
Tumia kunywa glasi tatu asubuhi, tatu mchana,tatu jioni kwa muda wa siku 15.
Utakuwa unafanya hivyo kila mara utakapo hitaji kuongeza maziwa.
๐๐๐ฎ ๐ง๐ถ๐ฏ๐ฎ ๐๐ถ๐น๐ถ๐๐ผ๐ฎ๐ป๐ฑ๐ฎ๐น๐ถ๐๐ฎ ๐ธ๐ถ๐๐ฎ๐ฎ๐น๐ฎ๐บ๐ Na Bei Tofauti
๐ช๐ฎ๐๐ถ๐น๐ถ๐ฎ๐ป๐ฎ
๐๐ก๐๐ญ๐ฌ๐๐ฉ๐ฉ / ๐๐๐ฅ๐ฅ / ๐ฌ๐ฆ๐ฌ +255734612449
https://mkitotanzania.blogspot.com/2022/02/tiba-asilia-zisizo-na-madhara-yoyote.html?m=1
Comments
Post a Comment